Na Anitha Jonas – WHUSM,Geita
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi wadau wa sekta ya filamu  Mkoa wa Geita kufikisha  maombi yao ya kupatiwa stika za TRA kwa kazi zao kwa watendaji wakuu wa TRA iliwaweze kupatiwa stika hizo katika ofisi ya TRA za  mkoani hapo.
 Mheshimiwa Mwakyembe ametoa ahadi hiyo leo mkoani Geita katika kikao na wadau wa kisekta wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo kikao hicho kililenga  la kupata taarifa na kujua changamoto za wadau hao ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki.
“Katika sekta ya Filamu nitazungumza na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania ili aweze kufika mkoani hapa na timu yake kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kuandaa miswada ya kazi za filamu kwani changamoto kubwa katika sekta ya filamu ni kuwepo na kazi nyingi zisizo na ubora,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza na wadau hao Waziri huyo alieleza kuwa serikali kupita idara yake ya Sanaa inaangalia namna ya kutafuta wafadhili watakao toa ufadhili wa kulipia mafunzo ya huduma katika ndege ili washindi wa mashindano ya urembo waweze kupata kazi ya kutoa huduma katika  Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Pamoja na hayo nae Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas alitoa elimu ya matumizi ya sheria mbili  ambazo ni Sheria ya Haki yakupata taarifa ya mwaka 2016 na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016,ambapo sheria hizi zinazohusu sekta ya habari na kuwafafanulia waandishi wa habari mipaka yao katika mambo ya kuyatolea habari ikiwemo mambo yanayohusu usalama wa taifa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wadau wa kisekta wa Mkoa wa Geita leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli zao na kujua changamoto zao  ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki, kutoka kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas (kulia) akitoa ufafafuzi wa sheria mbili zinazohusu sekta ya habari ambazo ni Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa 2016 na Sheria ya Huduma za Habari 2016 leo Mkoani Geita katika kikao na wadau wakisekta kwa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.
 Miss Geita 2018 Joyce Magesa akizungumza mbele ya Mhe.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe leo Mkoani Geita katika kikao cha wadau wa kisekta  kuhusu dhamira yake ya kushirikiana na serikali kwa lengo la kufanya kazi za kijamii kama Kauli Mbiu ya Mashindano ya Ulimbwende Duniani mwaka 2018 inavyoelekeza kuwa ni “Urembo na Kazi kwa Maendeleo ya Jamii” nyuma yake kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Wadau wa Michezo Mkoa wa Geita wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (aliyeketi watatu kushoto) mara baada ya kikao na wadau wa kisekta kilichofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Geita leo ,wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel  na watatu kulia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...