Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Wizara ya Maliasili na Utalii Nchini imezindua  rasmi kampeni ya kufanya usafi katika maeneo ya fukwe kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na  Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo pamoja na kufanya usafi kwenye Fukwe ya Hotel ya Ramada Resort, Mkurugenzi Msaidizi Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma amesema kuwa utaratibu huu uliowekwa na Bodi ya Utalii Nchini ya kufanya usafi kutasaidia kuboresha na kuvutia watalii wengi zaidi.

Rosada ambaye ameshiriki kusafisha ufukwe wa Ramada Resort, amesema ana imani kampeni hiyo itakuwa endelevu kwani ni miongoni mwa mipango ya Serikali kuvutia utalii wa fukwe."Tutakapokuwa tunafanya usafi kwenye fukwe zetu,  zikiwa safi kiukweli zitavutia utalii na watalii wengi watakuja kutoka sehemu mbalimbali kwa wanaopenda matembezi lakini pia kwa wazawa ni fursa ya kufanya biashara,” amesema Rosada.

Rosada amesema kuwa, wao kama Wizara ya Maliasili zoezi la usafi walilizindua Mwezi April mwaka huu wakiwa na lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuvutia watalii nchini.Mkurugenzi wa masoko wa TTB, Ernest Mwamaja amesema fukwe nyingi hazipo katika hali ya usafi na uchafu wake kwa asilimia kubwa ni makopo ya plastiki yanayoletwa na maji yanayotiririka kutoka kwa wananchi sehemu mbalimbali wanaotupa kwenye vyanzo vya maji kama vile mito.
Mkurugenzi Msaidizi wa Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.
 Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) Godfrey Meena akiwa sambamba na Kamishna msaidizi wa Polisi Makao Makuu Ferdinand Mtui wakishiriki usafi kafika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli ya Ramada Resort Bharath Swarup akiwa anashiriki usafi  katika uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania ( TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.


Wananchi na wafanyakazi mbalimbali wa Bodi ya Utalii na Hoteli ya Ramada Resort wakiendelea na usafi wakati wa uzinduzi wa kampenk ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa  wazawa na wageni.

Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii (TTB) Ernest Mwamwaja  (katikatk) akiwa anafanya usafi wakati wa kampeni ya uzinduzi ya kufanya usafu katika fukwe za bahari  kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort. Picha ya chini akiwa anazungumza na wanahabari baada ya kumaliza usafi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
http://michuzijr.blogspot.com/2018/08/wizara-ya-maliasili-na-utalii-yazindua.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...