Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKIRUGENZI Mtendaji wa timu ya Arusha United Saad Kawemba amesema kuwa kwa sasa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kuanza ligi daraja la kwanza baada ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao lkilichorejea jana kutokea mkoa wa Lindi, Kawemba amesema walikuwa wamepanga kuweka maandalizi ya kikosi chao katika mikoa 2 ambayo ni Dar es Salaam na Tanga na kucheza mechi za kirafiki ila wakabahatika na kuongeza mkoa mwingine ambao ni Lindi.

Kawemba amesema kuwa, wameweza kucheza mechi sita za kirafiki na katika michezo hiyo walifanikiwa kushinda michezo miwili na kutoa sare moja na mitatu wakipoteza.

Amesema kuwa, walianza mechi ya kwanza ya kirafiki na Simba ambapo walipoteza mchezo huo, walicheza pia na Coastal Union ya Tanga na mechi zingine wakicheza Lindi na Dar es Salaam na mchezo mwingine watacheza alhamisi dhidi ya Namungo ya Arusha.

Kawemba amewataka wana Arusha kuwa na imani na timu kwani wana uhakika wa kuoanda ligi kuu msimu ujao kutokana na kikosi kuwa kizuri na ushindani, akielezea kuwa kupoteza mechi yoyote katika mchezo wa kirafiki sio kama wana timu isiyo ya ushindani bali mwalimu anakuwa anaangalia makosa yaliyopo ili aweze kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa ligi.

"Tumecheza michezo sita ya kirafiki na Alhamisi tutacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Namungo na mechi hizo zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kikosi chetu kwani zimeweza kumsaidia Mwalimu kuona makosa yaliyopo kabla ya kuanza kwa ligi na kupoteza mechi ya kirafiki haimaanishi kuwa kikosi ni kibaya ila tuna imani na timu yetu mwakani itashiriki ligi kuu Tanzania bara,"amesema Kawemba.

Akizungumzia udhamini wa timu yao, Kawemba amewataka wadau mbalimbali wanaopendelea soka na wasio wajitokeze kuidhamini timu hiyo kwani kwa sasa kwani itakapopanda ligi kuu msimu ujao thamani yao itapanda zaidi.

Arusha United iliyo chini ya kocha Fred Felix Minziro akiwa na historia ya kuzipandisha timu za ligi daraja la kwanza katika kipindi mitatu uongozi wa timu hiyo umekuwa na imani kuwa msimu ujao kuwa timu yao itaingia Ligi Kuu.Minziro amefanikisjha timu ya Singida United, KMC kupanda ligi kuu katika misimu miwili tofauti.
MkuruenziMtendaji wa timu ya Arusha United Saad Kawemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...