Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Azam FC,kimefika salama  mkoani Shinyanga tayari kabisa kwa mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mwadui utakaofanyika Uwanja wa Mwadui Complex keshokutwa Ijumaa saa 8.00 mchana.


Azam FC imewasili ikiwa na kikosi chake kamili isipokuwa kiungo mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, atayeungana na timu muda wowote kaunzia sasa akitokea kwenye majukumu ya timu ya timu yake ya Taifa Zimbabwe.

Wachezaji wengine wa Azam FC ambao hawajaungana na timu ni mshambuliaji Wazir Junior pamoja na beki Yakubu Mohammed na Donald Ngoma, ambao wanaendelea na programu ya kujiweka fiti kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani wakitoka kwenye majeraha huku Joseph Kimwaga, akiwa majeruhi.


"Wachezaji wote wameshaungana na timu isipokuwa Tafadzwa Kutinyu ambaye ataungana na wenzake muda wowote atakuja na ndege hadi Dar es Salaam halafu ataunganisha mpaka Mwanza na baadae kuja kuungana na wenzie hapa Shinyanga,"amesema Iddy.

Iddy amesema kuwa, baada ya mchezo huo bado wana mechi zingine mbili katika kanda ya Ziwa wakicheza na Biashara ya Mara na kuja kumalizia na Alliance kabla ya kurejea Dar es Salaam.


Mara baada ya kuwasili, kikosi hicho kinatarajia kufanya mazoezi leo Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa kabla ya kesho Alhamisi kujifua tena katika Uwanja wa Mwadui itakaochezea mchezo huo, unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake.


Azam FC  inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na pointi sita ikishinda mechi mbili za awali ilizocheza, ikizidiwa pointi moja na Mbao inayoongoza kileleni ikiwa na pointi saba lakini ikicheza mechi moja zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...