Na  Bashir  Yakub
Sio siri wengi waliowekeza kwenye biashara ya bajaji,bodaboda,taxi na hata daladala wamejuta kufanya hivyo. Wengi wameingia hasara na mambo hayakuwa kama walivyotarajia. Na niamini,waliomo leo kwenye hiyo biashara sio wale walioanza, bali ni wageni kwani walioanza walishaacha siku nyingi kuepuka kichwa kuuma.
Sasa yafaa tuzingatie mambo kadhaa ya kisheria ili kuona  namna gani unaweza kudhibiti biashara hii na hata ikikushinda isikushinde ukiwa mwenye kupoteza(looser).Katika kufanya hivyo tutizama mambo mawili, kwanza Mkataba, na pili Udhamini.
1.MKATABA.
Eneo la mkataba au makubaliano ni eneo muhimu  sana tangu unapowaza biashara hii. Mkataba ndiyo tafsiri ya uhusiano wako na huyo unayemkabidhi chombo. Popote, na wakati wowote mtakapotofautiana  rejea yenu ya kwanza ni mkataba. Mkataba ndio biashara yenyewe, na hivyo uimara wa mkataba utatambulisha uimara wa biashara, halikadhalika udhaifu wa mkataba huenda ukawa ndio udhaifu wa biashara.
Na uimara wa mkataba ni sehemu kuu mbili. Kwanza mfumo, na pili maudhui/vipengele. Mfumo ni lazima mkataba uwe katika muundo mzuri wa sheria. Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba, Sura ya 345 kinasema mkataba  mzuri ni ule ambao umefanywa na watu stahili kufanya mkataba(partie’s competence), wenye hiari huru(free consent), wakibadilishana vitu halali(lawful object and consideration ), na kile wanachokubaliana kiwe hakijakatazwa na sheria nyingine yoyote. Kwahiyo mfumo mzuri wa mkataba utategemea haya.                  KUSOMA ZAIDI NENDA sheriayakub.blogspot.com



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...