Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ameitaka benki ya biashara ya CBA kuendelea kuwawezesha watanzania, hususani wa chini wapatao milioni  7.5 kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Dk. Mengi alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo mjini Dar es salaam ambapo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Pamoja na historia ndefu ya benki hiyo ilivyoanzishwa na baadae kuhamishia makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, Dk. Mengi alisema benki hiyo ina wajibu mkubwa wa kuwezesha kundi kubwa la watanzania kuukataa umaskini.
Dk. Mengi ambaye ametoa kitabu kinachoonesha jinsi ya kukabiliana na umaskini na ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF, amesema amevutiwa na mpango wa Benki hiyo wa kuwapatia mikopo watu wa kawaida sana kupitia mpango wake wa kuweka akiba kupitia simu za mikononi ujulikanao kama M- Pawa.
Alisema anaamini kama benki imedhamiria na kujiamini wanaweza kujipatia mafanikio makubwa kupitia falsafa ya ninaweza. Anasema njia ya dhamira ya kwamba mtu anaweza hakuna cha maana kinachoweza kufanyika.
Mapema viongozi mbalimbali na waalikwa wakizungumzia huduma ya CBA tawi la Tanzania walisema kwamba inawasaidia sana hasa watu wa kipato cha chini na hivyo wanajihakikishia maendeleo kupitia M-pawa.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni ambaye ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya CBA (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi akitoa salamu za benki hiyo kwa wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumzia kazi za taasisi yake kabla ya kuendesha mnada wa vitu ili kuchangisha fedha za kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6 zilipatikana wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa gofu kutoka Zambia wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...