Na Mwandishi Wetu, MAELEZO

Beijing-CHINA

RAIS wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping amesema, Serikali ya nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na Afrika katika maeneo makubwa nane katika kipindi cha miaka mitatu ijayo itayojikita katika masuala ya viwanda, miundombinu, biashara, kilimo, ulinzi na usalama pamoja na mazingira. 

Akifungua Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Bara la Afrika (FOCAC) leo Beijing China na Rais Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo amesema katika masuala ya viwanda, uchumi wa Bara la Afrika na usafirishaji wa bidhaa utaendelea kupewa kipaumbele na Serikali ya China pamoja na makampuni yake yanahimizwa kuwekeza katika nchi za Afrika.

Kuhusu sekta ya kilimo, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga kuanzisha miradi 50 itayogharimu kiasi cha Yuan Bilioni 1 (Dola Milioni 147) itayosaidia masuala ya dharura na majanga mbalimbali ya kibinadamu sambamba na hilo, Rais Xi Jinping ameahidi kupeleka wataalamu 500 wa masuala ya kilimo ili kusaidia maendeleo ya sekta hiyo Barani Afrika.

Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu, Rais Xi Jinping amesema Serikali ya China itafanya juhudi na Umoja wa Afrika kuunda mpango wa ushirikiano wa Miundombinu baina ya Bara la Afrika na China na kusaidia makampuni ya Serikali ya China kupata fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...