Na Beatrice Lyimo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali katika sekta ya afya kuleta matokeo chanya yanayokusudiwa na Serikali.

Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo  Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Pili la Tathmini na Ufutiliaji lililloandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Calfonia  cha Marekani likilenga kujadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kutumia matokeo ya tafiti za sekta ya afya kufanya tathmini na ufuatiliaji ili kuimarisha huduma zinazotolewa.

"Tuhakikishe rasilimali fedha inayowekezwa katika sekta ya afya inatumika vizuri ili kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa na pia mfanye taafiti zitakazo saidia kuboresha na kusimamia sera na maamuzi ya Serikali" ameongeza Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt Ndugulile, amekiasa Chuo hicho kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wadau mbalimbali wanayojishughulisha na masuala ya afya kwa lengo la kuibua changamoto na  kufanya utafiti ili kutoa majibu ambayo Serikali na wadau wanayahitaji ili kutoa majawabu kwa kuchukua hatua stahiki.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kupeana uzoefu kuhusu umuhimu wa ufuatiliaji na tathimini katika sekta ya afya.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka  wakati wa Kongamano la pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali wakiwemo wanafunzi na Watafiti.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka  akizungumzia nafasi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika kufanikisha programu mbalimbali za tafiti hasa katika sekta ya afya na kuzichakata taarifa zinazokusanywa ili zisaidie watunga sera katika kufanya maamuzi.
  Sehemu ya washiriki wa Kongamano  la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi  wa Chuo Kikuu Mzumbe  na Watafiti.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...