Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUUwa Wilaya ya Biharamulo Sada Malunde amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria.

Malunde ametoa agizo hilo jana Septemba 23 akiwa kwenye msitu wa Nyantakara ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuona uvamizi na uharibifu mkubwa unaoendelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo.

“Misitu huu unavamiwa kwa kasi kubwa na kuharibiwa na watu wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria, hali hii inatishia zaidi baada ya Serikali kupandisha hadhi mapori tengefu ya Kimisi, Burigi na Biharamulo kuwa Hifadhi za Taifa ambapo kuna sheria kali zinazowabana wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

"Nikiwa kama kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria. Sitakubali hali hii iendelee, nawataka muondoke kwa hiari na kwenda kuishi kwenye vijiji vinavyotambulika kisheria kabla selikali hajatumia nguvu kuwaondoa,” amesema Malunde.Aidha Malunde alisema ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuangalia uwezekano wakurekebisha sheria za misitu na kuzifanya ziwe kali zaidi ili kuepuka uharibifu wa hifadhi za misitu nchini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Professa Dos Santos Silayo amesema kuwa vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya misitu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na kuahidi kushirikiana kikamilifu kudhibiti uvamizi na uharibifu wa misitu wilayani huo.Kwa upande wa Meneja Misitu wa Kanda ya Ziwa Cosmas Ndakidemi amewataka wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuheshimu mipaka na taratibu zilizopo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria.

Tayari kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ilishatoa maagizo kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi ya misitu kuondoka kabla ya mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu.
Kulia ni Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Emmanuel Komba akimweleza Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Dos Santos Silayo (aliyeshika kiunx) jinsi wavamizi wa maeneo ya msitu wa Nyantakara wilayani humo wanavyathiri uhifadhi na kuhujumu uchumi wa Taifa walipotembelea situ huo na kujionea uharibifu mkubwa wa msitu huo unaosababishwa na shughuli za uchomaji mkaa . Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde (mwenye kofia) akiwataka wananchi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria alipokuwa kwenye Kijiji cha Mpago kilichopo ndani ya msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo jana. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Professa Dos Santos Silayo mwenye dhamana ya kusimamia msitu huo.
Mmoja kati ya wavamizi wa msitu (hakuweza kufahamika jina lake) wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo akiendelea na shughuli zake katika msitu huo licha ya kutakiwa kuondoka mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kama alivyokutwa na mpiga picha wetu katika Kijiji cha Nyamagana kilichopo ndani ya msitu huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...