NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu na waache mara moja ,kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina yao na wakulima.

Aidha, amepiga marufuku wafugaji kuingiza mifugo yao kiholela wilayani humo pamoja na maeneo ya wawekezaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara. 
Rai hiyo aliitoa ,wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo. 

DC Zainab alieleza  kuwa wapo viongozi wanaokula na wafugaji suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi. 

Alisema kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano.

“Nasema inatosha, wilaya kwasasa ina mifugo hiyo 300,000 yaani halmashauri ya Chalinze ina ng'ombe 240,000 na Bagamoyo ng'ombe 60, 000,"

Zainab alielezea, baaadhi ya viongozi wamekuwa wakijihusisha na uingizaji mifugo kwa kutumia njia ambazo ni kinyume cha sheria hali ambayo inasababisha madhara makubwa ndani ya jamii .
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa akizungumza na watendaji na madiwani. 
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya watendaji na madiwani wa Bagamoyo wakifuatilia yaliyojiri kwenye kikao cha baraza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...