Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
DEREVA wa bodaboda aliyetambulika kwa jina la Msafiri mkazi wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ameshinda bajaji baada ya kuibuka mshindi katika droo ya  Sportpesa.

Imeelezwa kuwa mshindi huyo ni wa kwanza baada ya Sportspesa kuzindua rasmi shindano la Shida zaidi na Sportspesa jana.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportspesa Abbas Tarimba ameeleza furaha ya kumpata mshindi huyo kwa mara ya kwanza  ambaye ametokea mkoani Tanga.

Tarimba ametoa rai kwa washiriki kuendelea kubashiri kwa wingi zaidi ili kujiwekea nafasi ya  kuingia kwenye droo na kubadilisha maisha yao kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Martin
Langarivo amempongeza mshindi huyo mwenye umri wa miaka 21.

Ametoa rai kwa  wengine kushiriki kwani ni mchezo ambao unafata masharti yote ya bodi pamoja na kutenda haki kwa washindi na hakuna mtu ambae anapangwa kama watu wanavosema .

Kwa mujibu wa Sportspesa ni kwamba baada ya bajaji hiyo kupata mshindi sasa zimebaki bajaji 99 ambazo zinasubiri washindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...