Na Veronica Kazimoto Manyara.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi kwa wafanyabiashara, washauri wa wafanyabiashara na wakaguzi wa hesabu mkoani Manyara ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wale wote wenye madeni ya kodi yanayotokana na riba na adhabu kuomba msamaha kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.



Akiwasilisha mada kuhusu msamaha huo, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amesema kuwa, lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kwamba, kila mfanyabiashara mwenye malimbikizo ya madeni ya kodi anapata taarifa na kufuata taratibu za kuomba msamaha huo.

"Mpaka sasa TRA imeshatoa elimu hii ya msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi katika mikoa mingi nchini na lengo letu ni kuwahamasisha wafanyabiashara wote wenye malimbikizo hayo kuomba msamaha ili waweze kupata unafuu na kulipa kodi ya msingi tu isiyo na riba wala adhabu," alisema Masalla.

Aidha, pamoja na washiriki hao kupewa elimu ya msamaha wa riba na adhabu ya kodi, pia wameelimishwa kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza akizungumza na washiriki hao wakati akiwasilisha mada ya maadili amesema kuwa, ni haki ya wateja wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhudumiwa vizuri na kwa usawa bila upendeleo.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akitoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
 Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
 Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Manyara Nicodemus Massawe akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabishara wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara.

Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...