Na Lusungu Helela
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya Kisasa, Maafisa wanyamapori watakuwa na uwezo wa kuwaona faru popote walipo wakati wakiwa wamekaa ofisini hali itakayosaidia kuwalinda wanyamapori hao ambao wapo hatarini kutoweka.

Pia amesema Maofisa hao watakuwa na uwezo wa kufuatilia mienendo ya wanyama hao pale walipo na popote wanapoenda ili kujua kama wanaumwa au wanatatizo lolote hali itakayosaidia kwenda kutoa huduma ili wanyama hao waendelee kuishi. 

 Mhe. Hasunga amezungumza hayo alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mara baada ya kushuhudia zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
 Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwenye uhifadhi wa wanyamapori hali itakayopelekea majangili kukamatwa hata kabla hawajamuua faru. 

 Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa faru katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Phillibert Ngoti amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa zoezi hilo la uwekaji alama za vifaa vya kisasa unafanywa katika Hifadhi hiyo kwa kushirikina na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA) Frunkfurt Zoological Society( FZS) pamoja Friedkin Conservation Fund ( FCF) .

 Bwana Ngoti amefafanua kuwa zoezi la uwekaji wa vitambuzi hivyo kwenye faru unafanyika kwa namna mbili, kuna vitambuzi vinavyowekwa ndani ya pembe za faru na pia kuna vitambuzi vinavyowekwa kwenye mguu mmoja wa mbele wa faru ili kusaidia kujua popote pale walipo. 

 Kwa upande wake, Kiongozi wa Mradi wa Uhifadhi kutoka FZS, Rian Habuschagne amesema mradi huo umefadhiliwa na Frunkfurt Zoological Society kwa kushirikiana na Friedkin Conservation Society. 

 Bwana Habuschagne ameeleza kuwa, wameweza kusaidia helkopta, mahema, kumlipa rubani, chakula kwa askari wanyamapori pamoja na magari na hadi kukamilika kwa mradi huo unaweza kugharimu zaidi ya bilioni moja. 

 Ameongeza kuwa utaratibu wa uwekaji vitambuzi kwa faru umekuwa pia ukifanyika nchini Afrika Kusini hali iliyosaidia sana katika kuwalinda faru. Aidha, Daktari wa Wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Alex Muse anayeshiriki katika zoezi hilo amesema kuwa zoezi la uwekaji vitambuzi kwa faru lina changamoto zake lakini kwa vile kuna timu nzuri kwa ajili ya kazi hiyo hivyo imekuwa kazi nyepesi kwao.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akishiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akishiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akiwa na wataalamu na askari wa wanyamapori baada ka kushiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Faru akipozwa na maji katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...