Mkuu wa Idara ya  huduma za tiba radiolojia (Interventional Radiology) Dkt. Frolence Lwakatare (katikati) akiongea na wanahabari wakati akielezea jinsi huduma hiyo ilivyo muhimu kwa jamii ambalo amesema kuwa inapunguza hatari kwa mgonjwa maana upasuaji huwa unahatarisha maisha ya mgonjwa. Kulia ni Joan mmoja ya wagonjwa walipatiwa matibabu na Kushoto ni Daktari Bingwa wa Meno, Kimywa na Uso, Dkt. William Siang'a.
Mkurugenzi wa wa huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Agweyo (katikati) akiongea na wanahabari kuelezea huduma mpya walioyoianzisha tokea Novemba 2017 inahusisha utalaam wa kutumia vifaa vya radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra-Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.  Kulia ni Joan mmoja ya wagonjwa waliopatiwa matibabu na (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya  huduma za tiba radiolojia (Interventional Radiology) Dkt. Frolence Lwakatare. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Daktari Bingwa wa Meno, Kimywa na Uso, Dkt. William Siang'a akieleza machache.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
*Wagonjwa 45 wahudumiwa, wagharimu Tshs. 360 Mil. badala ya Tshs. 4.320 Bil kama wangeenda nje ya nchi

*Mmoja agharimu Tshs. 8 Mil. badala ya Tshs. 96 Mil. nje ya nchi

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanzisha kwa mara ya kwanza hapa nchini utoaji wa huduma za tiba radiolojia (Interventional Radiology) ambapo kabla ya uanzishwaji wake wagonjwa waliokuwa wanahitaji huduma hizi walikuwa wakienda nje ya nchi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akielezea kuanzishwa wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa wa huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Agweyo amesema kuwa tiba hiyo inahusisha utalaam wa kutumia vifaa vya radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra-Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Amesema kuwa huduma ambazo zimeanza kutolewa kupitia njia hiyo kwa sasa ni kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingoni (sclerotherapy for haemangioma and lymphangioma), kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya kutoa mkojo imeziba (nephrostomy tube placement), kuzibua mirija ya nyongo iliyoziba (percutaneous trans hepatic biliary drainage) na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba (fallopian tube recanalization). Tiba nyingine ni kunyonya usaha ndani ya tumbo (abscesses drainage).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...