* Ni katika tukio la kuzama kivuko cha MV.Nyerere, Mbunge wa Ukerewe aomba kivuko cha uhakika

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema msiba huo ni mkubwa na wa kitaifa huku akieleza kuwa wananchi wamefanya kazi kubwa kwani wao ndio wamefanikisha kupata kwa watu 40 walio hai.

Mongella amesema hayo leo mchana huu wakati akitambulisha viongozi mbalimbali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameongoza maziko ya Watanzania waliopoteza maisha kutokana na tukio la kupinduka kwa kivuko cha Mv.Nyerere.

Mkuu huyo wa Mkoa amemwambia Waziri Mkuu kwamba Septemba 20 mwaka huu saa nane mchana walipata taarifa za kuwa kivuko hicho kinazama na wao wakafika eneo la tukio saa 11 jioni.

Amesema baada ya kufika walikuwa wananchi wa eneo hilo tayari wamefanikiwa kuokoa watu walio hai 40 na hakika wananchi hao wamefanya kazi kubwa."Watu 40 wameokolewa na wananchi wa maeneo haya.Sisi wengine wote tumeokoa mtu mmoja tu jana.Hivyo wananchi hawa wamethibitisha uwezo mkubwa na tunao watu wananchi wenye uwezo mkubwa," amesema.

Wakati huo huo Mongella amesema kwamba tukio hilo limeacha majonzi na masikitiko makubwa lakini wanashukuru ushiriki wa makundi mbalimbali kwa namna ambavyo wameshiriki katika tukio hilo.Pia wamesema  viongozi mbalimbali nao wamefika katika eneo la tukio hilo na uwepo wao umekuwa faraja kubwa.

"Kwa namna ambavyo watu wameshiriki katika tukio hilo ni vema tukashukuru makundi yote na si mtu mmoja mmoja," amesema Mongella.


MBUNGE WA UKEREWE

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi (Chadema) amemwambia Waziri Mkuu kwamba amejawa na simanzi kutokana na tukio hilo.Pia amesema katika maisha yake hakuwahi kushuhudia vifo vya idadi kubwa kwa mara moja kama ambavyo imetoke huku akieleza  na tukio hilo ni janga ambalo tayari limetokea.

Amesema kutokana na  janga hilo kuna jambo la kujifunza kuhakikisha halitokei tena tukio la aina hiyo huku akiomba Watanzania kushikamana kama Taifa."Faraja ambayo tunayoweza kuipata sisi wananchi wa Ukerewe na ukanda huu ni kupata chombo ambacho kitakuwa madhubuti na kuhakikisha wananchi wa eneo hili maisha yao kuwa salama.

" Tuwaombee marehemu wetu roho zao Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema peponi.Amina,"amesema Mbunge huyo.

VIONGOZI WA DINI

Kabla ya kuipumzisha miili hiyo Katika nyumba zao za milele viongozi wa dini zote wameleza kusikitishwa na tukio hilo na kuomba dua na sala kwa Mwenyezi Mungu kutokana na tukio hilo.ia viongozi hao pamoja na kumuomba Mungu awape faraja wafiwa ambao wameondokewa na wapendwa wao wameeleza kwamba tukio limeleta masikitiko makubwa lakini wanaamini kila jambo jambo hupangwa na Mungu.

Wamefafanua watu wamekusanyika hapo ili kushuhudia tukio kubwa la kuwasitiri wapendwa wetu ambao leo wanarudi mavumbi.Pia wamuomba Mungu awape faraja viongozi wa ngazi mbalimbali katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa linapitia.

Viongozi hao wamesema wanawaombea wote walioaga dunia wasamehewe zambi zao.Wameomba Mungu aliupushe Taifa na majanga ambayo yanaweza kutokea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...