Na Said Mwishehe,Globu ya kamii 
 KIVUKO cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kimezama katika ziwa Victoria.
Inadaiwa kwamba kivuko hicho kimezama kikiwa na abiria ambapo hata hivyo bado haijafahamika idadi ya abiria waliokuwemo ingawa taarifa za awali zinadai kilikuwa na abiria zaidi ya 90. Kwa mujibu wa baadhi ya waliozungumzia kivuko hicho wamedai kilikuwa kinatokea Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye gati ya Ukara. 
 Kwa mujibu wa nashuhuda wamedai kuwa ghafla kilianza kutitia kwenye maji kwa nyuma kulikokuwa na mzigo na kuwezesha abiria waliokuwa mbele kurukia majini na kuogelea na mitumbwi iliyokuwa pale kufanya kazi ya kuwaokoa abiria waliorukia majini. 
 Pia inadaiwa abiria wengi waliokuwa ndani ya Mv Nyerere hawakuweza kutoka na kuwa wamezama. Mmoja ya waliozungumzia kuzama kwa kivuko hicho amedai idadi ya abiria waliopanda haijulikani ingawa uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 150. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikifanikiwa kwani simu yake haikuwa hewani. 
 Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kupigiwa simu ya mkononi alisema yupo kikaoni. Hivyo tutaendelea kuwajuza kinachoendelea na idadi kamili ua abiria waliokuwamo kwenye kivuko hicho. 
 Wakati huo huo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo chini ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano umesema unasikitishwa na tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere. Kivuko hicho kimekuwa kinatoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Ukara na Bugolora wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. 
 Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari naKitengo cha Habari na Mawasiliano cha TEMESA imesema wanasikitishwa na ajali hiyo na inawaomba wananchi wote kuwa na subira wakati taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la kusikitisha zikiendelea kutolewa.

Wananchi wakiwa kwenye ufukwe wa Ukara wakishuhudia  uokoaji wa abiria waliokuwamo katika kivuko cha MV Nyerere 
Juhudi za uokoaji zikifanyika
Picha ya maktaba ya kivuko cha MV Nyerere 


Picha ya maktaba ya kivuko cha MV Nyerere 
Picha na G. Sengo wa Jembe FM, Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...