Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyeketi kushoto) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyechuchumaa) wakizindua kazi ya kutandika reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga, Pwani. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati) akikagua kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR, Soga mkoani Pwani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa tatu kulia) akipata maelezo ya namna ya kutengeneza mataruma ya reli ya kisasa ya SGR kwenye kIiwanda cha Soga, Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na wa kawanza kushoto ni Farid Munir Abdallah, Mhandisi Mzalishaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) namna kazi ya utandikaji reli ya kisasa ya SGR inavyofanyika kwenye eneo la Soga mkoa wa Pwani 
Mmoja wa mafundi wakiendelea na kazi ya kutengeneza mataruma ya kujengea reli ya kisasa ya SGR kwenye iwanda cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua rasmi kazi ya utandikaji wa reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga lililopo mkoani Pwani ambapo reli hiyo inajengwa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa umbali wa kilomita 300 na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa.

Kamwelwe amesema kuwa reli hiyo yenye jumla ya kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni kwa ajili ya njia ya reli ambayo itakuwa na umbali wa kilomita 205 na kilomita 95 ni kwa ajili ya reli kupishana ambapo reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo kiasi cha tani milioni 17,000 kwa mwaka ambapo nchi yetu imeingia mkataba wa kujenga reli hiyo na kampuni ya Yapi Merkezi ya kutoka nchini Uturuki na kusimamiwa na mshauri mwelekezi wa kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya hapa nchini kwetu. Reli hiyo itaendeshwa kwa kutumia umeme na itakuwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa.

Ameongeza kuwa Serikali inazalisha mataruma kwenye kiwanda chake yenyewe kilichopo Soga mkoa wa Pwani na vifaa vingine vya ujenzi wa reli hiyo kama vile sementi, mchanga na kokoto vyote vinapatikana hapa nchini. Amefafanua kuwa Serikali iliagiza reli peke yake kutoka nchini Japan ambapo kiasi cha tani 7,250 ziliingizwa nchini katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo reli hizo zitatumika kujenga reli hiyo ya kisasa ya SGR kwa ukubwa wa kilomita 60. Amesema kuwa itafika siku ambapo nchi itachimba chuma kutoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa ya SGR badala ya kuendelea kuagiza reli kutoka nje ya nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...