Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
MWILI wa aliyekuwa katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan (80) aliyefariki dunia Agosti 18 katika hospitali ya Bern nchini Uswizi baada ya kuugua kwa muda mfupi utazikwa leo katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Baada ya kuagwa kwa siku mbili na kumalizika kwa taratibu za kimila, Kofi atapumzishwa kwenye makaburi ya jeshi nchini humo, Marais wastaafu wa nchi za Ujerumani, Finland na Uswizi watashiriki katika kumpumzisha kiongozi hiyo.

Rais wa nchi hiyo Nana Akufo Addo ameeleza kuwa msiba huo ni wa kitaifa na hii ni kutokana na mchango mkubwa wa kiongozi huyo katika bara la Afrika, Pia Marais wa nchi jirani za Ivory coast, Liberia, Namibia, Ethiopia na Niger wamethibitisha kuhudhuria katika mazishi hayo. 

Kofi alikuwa mwafrika wa kwanza kutoka Kumasi nchini Ghana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na alihudumu kwa awamu mbili kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2016.

Kofi alizaliwa  Aprili 8, 1938 huko Kumasi nchini Ghana na alisoma taaluma mbalimbali ikiwe Uchumi aliyosoma katika Chuo cha Macalester na Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Geneva na alianza kuitumikia UN mwaka 1962 katika shirika la afya duniani  (WHO.) Na ameshinda tuzo mbalimbali ikiwemo ya kulinda amani 2001.

Kofi ameacha mke (bi Nane Maria Annan) na watoto (Kojo, Ama na Nina) ambao walikuwa karibu naye  hadi umauti unamfika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...