Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, ambao walifika kituoni hapo kuripoti matukio mbalimbali. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo,ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Wapili kulia ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akihoji makosa ya watuhumiwa mbalimbali (hawapo pichani) waliopo katika mahabusu ya Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, leo. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Katikati ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akiyaangalia kwa makini orodha ya majina ya watuhumiwa na makosa yao ambao wapo mahabusu ya kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, leo, wakati askari polisi wa kituo hicho, Janeth Shushu alipomletea kitabu cha taarifa mbalimbali za makosa yaliyoripotiwa kituoni hapo. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Katikati ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Askari wa usalama barabarani wa Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, Alau Mawanda (kushoto) akimuonyesha risiti Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), ambayo askari huyo alimkatia Dereva wa gari ndogo (hayupo pichani), baada ya kuvunja sheria za usalama barabani. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Kulia ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...