Na Agness Francis globu ya jamii
KAMPUNI ya mchezo wa kubahatisha M- Bet imeendelea kutoa zawadi kwa wateja wao ambao wamekuwa waotumia fursa ya kubeti mchezo wa kubahatisha.

Ambapo leo M Bet wametoa  hundi ya Sh. milioni 7.7 kwa mshindi ambaye ni wa 2  kwa mwezi huu wa droo  ya Perfect 12 .Mshindi huyo ametajwa kwa jina la  Given Mgale Mkazi wa Kagera.

Akizungumza leo Ofisa Habari wa M- Bet David Malley amesema baada ya ushindi huo na kukabidhi zawadi Serikali itachukua kiasi cha asilimia 14  ambayo ni kodi na mshindi wao atakabidhiwa  zaidi ya Sh.Milioni 56.

Hata hivyo Malley amewaomba watu watumie fursa ya kujaribu bahati zao  katika kushiriki droo hiyo kwa shilingi 1000 tu kwa kutumia njia ya Simu kwa kupiga *149*19#  na kwa wenye smartphone waingie tovuti ya www.m-bet.co.tz kisha kwenda sehemu yenye mchezo wa  perfect 12.

Kwa upande wake Mshindi huyo amesema haikuwa rahisi kwake kushinda kwani alijaribu kubeti mara nyingi zaidi na  hakukata tamaa kwa kuamini ipo siku ndoto zake zitatimia.

"Safari ya kushinda fedha hizo ilikuwa ndefu kidogo kwangu, lakini sikukata tamaa mpaka nilipotangazwa mshindi wa M-Bet droo ya perfect 12 September 17  na sasa ndoto zangu za kujenga nyumba na kufanya biashara  zimetimia.Nawashukuru vijana wenzangu watumie fursa wasikate tamaa,"amesema Given.
Afisa Habari wa kampuni ya M-Bet, David Malley(kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 70.7  Mshindi wa M-Bet, Given  Mgale (katikati)   leo jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa  mshindi wa 2 kwa mwezi huu katika  droo ya 17 ya perfect 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...