Na Mary Gwera, Mahakama

JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.

Mhe. Jaji Feleshi aliyasema hayo, Septemba 22 jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kuwaaga jumla ya Majaji Wastaafu tisa (9) kutoka Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi.

“Napenda kuwapongeza kwa Utumishi wenu uliotukuka kwa Mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa Mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Jaji Kiongozi. Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwataka Majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia Mpango Mkakati wake.

Aliongeza kwa kuwasihi Majaji hao Wastaafu kutosita kutoa ujuzi wao kwa Majaji ambao bado wapo kwenye Utumishi wa Umma pindi wanapohitajika kutoa elimu katika Mafunzo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Mahakama. Kwa upande wake, Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Fredrica Mgaya ameushukuru Uongozi wa Mahakama kwa kuwaandalia hafla hiyo kwani wamefurahi na kujisikia kuwa wao bado ni sehemu ya Wanafamilia wa Mahakama.

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo. 
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo. 
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Sekieth Kihio akipokea zawadi kutoka kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, (katikati) ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Jaji Mstaafu Mhe. Laurence Kaduri ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kumaliza utumishi wa Mahakama salama. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...