Na  Bashir  Yakub.

Kuna tofauti kati ya gharama za kesi(costs), fidia (compesation), na faini(fine). Gharama za kesi ni nje ya haya lakini pia ni nje ya kile ulichoshinda. Kwasababu imeamriwa ulipwe fidia au imeamriwa ulipwe faini haimaanishi hata gharama zinahesabika humohumo. Laa, hasha, kama ni fidia utalipwa, kadhalika na gharama utatakiwa  kulipwa.

Ukweli ni kuwa watu wengi huwa hawadai gharama za kesi . Mtu akishaambiwa ameshinda basi. Kama imeamriwa alipwe pesa, au kama ni mali kama ardhi imeamriwa arudishiwe, au ushindi mwingine wowote basi  huondoka tu moja kwa moja bila kudai gharama zake. Sasa yafaa ujue kuwa nje ya ushindi unaopewa na mahakama pia unatakiwa kulipwa gharama zako za kuendeshea shauri/kesi.

1.GHARAMA ZA KESI NI NINI .

Gharama za kesi ni yale matumizi yote halali uliyoingia wakati ukishughulikia kesi/shauri husika. Hizi ni pamoja na nauli ulizokuwa ukitumia kutoka nyumbani kwenda mahakamani kwa kipindi chote cha kesi/shauri mpaka kuisha,pesa uliyomlipa wakili kama ulikuwa unawakilishwa na wakili, pesa uliyotumia kumlipa wakili kuandaa nyaraka , pesa ya kuchapa(print),pesa ya  kutoa kopi kwenye nyaraka mbalimbali ulizokuwa ukiwasilisha mahakamani, na gharama nyingine yoyote ambayo uliingia wakati ukifuatilia kesi/shauri.

Isipokuwa tu gharama hizo ziwe zile ambazo ni halali. Rushwa na gharama nyingine za ajabu ambazo umeingia haziwezi kulipwa na ni makosa iwapo ulifanya hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...