Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kigoma ambapo ametembelea Wilaya ya Uvinza.

Akiwa Wilayani Uvinza, Makamu wa Rais aliweza kutembelea mwalo wa Muyobozi uliojengwa kwa gharama za shilingi milioni 482 na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kumlaki.

Pia alikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Kituo cha Afya Uvinza ambapo shilingi milioni 400 zimetolewa kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Upasuaji, Jengo la X-Ray, Jengo la Wazazi, Maabara na Nyumba ya Mtumishi.

Mradi huu unalenga kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wote wa Wilaya ya Uvinza hasa kwa akina Mama Wajawazito na Watoto na unatekelezwa kwa kutumia njia ya “Force Account”.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Ruchugi kitongoji cha Kibaoni, Makamu wa Rais aliwataka wananchi wa Kigoma kuzingatia lishe bora kwa watoto kwani mkoa una chakula cha kutosha.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewahimiza wananchi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao haswa wanaume pia aliwataka wananchi hao kutoa taarifa za wageni wanaonyesha kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kuchakata dagaa kutoka kwa mmoja wa wachakataji Bi. Mwajuma Bakari Shingo wakati alipotembelea mwalo wa Muyobozi uliopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Athuman mwenye umri wa wiki mbili aliyelazwa katika kituo cha afya cha Uvinza, aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto Esil Amour, Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya cha Uvinza ambapo kuna mradi wa upanuzi wa ujenzi wa kituo hicho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Ruchugi kitongoji cha Kibaoni ikiwa sehemu ya ziara yake wilayani Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...