Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Tabora katika viwanja vya Chipukizi kabla ya kuanza kutatua igogoro ya ardhi zao jana.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(hayupo katika picha)  wakati wa  ziara ya siku moja ya kiongozi huyo ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
 Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora ambao wana matatizo katika ardhi wakisubiri kukutana na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo katika picha ) ili asikilize shida zao wakati wa  ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
picha na Tiganya Vincent


NA TIGANYA VINCENT- RS TABORA
SERIKALI imepiga marufuku kampuni binafisi za upimaji ardhi  ambazo zimekuwa zikiingia makubaliano ya upimaji ardhi za wananachi bila hata uongozi wa Wilaya husika kuwa na taarifa juu ya uwepo wa zoezi hili hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kuwadhulumu fedha zao.

Agizo hili lilitolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi baada ya wakazi wa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora kuilalamikia Kampuni ya Ardhi Plan kuwachangisha fedha zao bila ya kupimia ardhi yao.

Alisema kuanzia sasa nchini kote hakuna Kampuni ya aina yoyote binafsi kwenda na kuingia moja kwa moja makubaliano na wananchi ya kuwapimia maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya husika.

Lukuvi alisema Kampuni za aina hiyo zimekuwa zikiwachangisha fedha na kugawana mapato bila hata ya kuwapimia wananchi huku uongozi wa Wilaya husika hauna hata taarifa.

Alisema haiwezekani upimaji wa ardhi za wanyonge ukageuza uchochoro wa kuwaibia na kuwadhulumu wananachi haki zao na kuongeza kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe katika upimaji wa ardhi za wananchi na taarifa ziwe kwa Wakuu wa Wilaya.

Aidha Waziri huyo alizitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia Chuo cha Ardhi Tabora na kuachana na Kampuni za nje kupima ardhi ili kuepuka matumizi makubwa ya gharama za zoezi hilo.

Alisema hakuna sababu ya Tabora kuendelea kuwa na maeneo ambayo yanajengwa kiholela holela wakati wanao wataalamu katika Chuo cha Ardhi ambao wameshindwa kuwatumia.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Lukuvi alizitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha maeneo yao wanayomiliki yamepima na wanazo hati kabla ya kumalizika kwa mwa mwaka huu.

Alisema baada ya kupima wanatakiwa kuweka alama katika mipaka ya maeneo yao ili kuepuka wananchi kuyavamia na kujenga na kusababisha migogoro ambayo inaweza kuzuilika.

Wakati huo huo Lukuvi ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanakamilisha uandaaji wa hati miliki za  viwanja 938 katika eneo la Malabi na kuwakabidhi wamiliki wake kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Alisema hatua ya kuendelea kukaa na viwanja hivyo bila kutoa hati kwa wahusika kwa miaka mitatu iliyopita kumesababishia hasara Serikali ya kukosa kodi ya ardhi kutoka kwa wahusika.

Waziri huyo aliwataka wakazi wa Malabi kuanzia Jumatatu ijayo ambao wameshipimiwa maeneo yao kwenda kuviripia ili hatimaye wapate hati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alikuwa katika ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi ambapo alifanikiwa kusikiliza migogoro ardhi zaidi ya 540 na kuipatai majibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...