Na Tiganya Vincent
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Serikali Mkoani Tabora kwa kufanya kazi zao kwa ushirikiano ambao umesaidia kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.
Alisema vyombo hivyo vinapaswa kuwa kitu kimoja jambo ambalo litawasaidia kubadilishana taarifa ili kufichua vikundi vya kihalifu kwa ajili ya kuhakikisha amani na salama miongoni mwa wananchi.
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Masanja alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi wa Serikali , Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipotembelea Ofisi ya Mkoa wa Tabora.
“Sio kila chombo kiende njia yake lazima kuwepo na umoja na mshikamano katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi” alisema.
Aliongeza kuwa na kila Wananchi analo jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi kwa kuchukua hatua za kutoa taarifa juu ya vikundi vya uhalifu katika maeneo yao ambazo zitaviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuzuia uhalifu.
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkaribisha Mkuu wa Utumishi
Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja ili aweze kuzungumza na
viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea
Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja akizungumza
na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala
Komaya(kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) na
Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa
Tabora.
Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya akuzungumza na viongozi mbalimbali
na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja
Jenerali Blasius Kalima Masanja alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa
Tabora.
Maofisa
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Tabora wakisikiliza Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja
Jenerali Blasius Kalima Masanja (hayupo katika picha) wakati
alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali Blasius Kalima Masanja akiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya( wa tatu
kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( wa tatu
kutoka kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa mara baada ya kutembelea
Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...