Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NI pigo!Ndivyo unavyoweza kuelezea taarifa za kufariki dunia kwa Mhadhiri wa  Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dk.Misanya Dismas Bingi.

Dk.Misanya ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji maarufu nchini  wa Radio One na ITV amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuz Blog Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbii Aminiel Aligaeshi amesema Dk.Misanya amefia MOI ila mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Muhimbili.

 Dk.Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.Alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili  baada ya kupata ugonjwa wa kupooza(stroke) na kupelekwa katika chumba cha Uangalizi maalum (ICU).

Kwa sasa msiba upo eneo la Makongo Juu jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea.Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea kuhusu msiba huo.

Pia Michuzi Blog inaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na msiba huo mzito wa kuondokewa na mendwa wao Dk.Misanya Bingi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...