Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara.
Katika mkutano huo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF.
Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
Wa kwanza pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
,Bwana William Erio akiwa kwenye
mazungumzo na Menejimenti ya Benki ya
CRDB ofisini kwake makao makuu jijini DSM ambapo wameweza kuzungumza masuala
mbali mbali ya kuimairisha mahusiano baina yao.
Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika
kwa mazungumzo yao kwenye makao makuu ya
NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni yake ni
mkurugenzi mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi mbalimbali wa CRDB na NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya UBA ,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake
na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio leo katika makao makuu ya
NSSF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya NMB Bi.Ineke
Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) Bwana William Erio (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar
es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Bwana
Miichael Mungure amabaye ni MKuu wa kitengo cha akaunti na malipo(NMB), wa
kwanza kulia ni Richard Mtapa ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za
Serikali(NMB)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...