Meneja wa Usimamizi wa Bima Kanda ya Nyamda za Juu kusini Consolata Gabone( katikati ) akikagua moja ya nyaraka za bima kutoka kwa mmiliki wa chombo cha moto katika neo la Stendi ya Nane nane jijini Mbeya.
Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa wamesimamisha magari ya abiri (daladala)katika eneo la stendi ya nanenane jijini Mbeya kwa lengo la kufanya ukaguzi wa bima za magari.
Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakifanya ukaguzi wa bima katika eneo la Stendi ya Daladala jijini Mbeya.

Na Emanuel Madafa,MichuziBlog - Mbeya 

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imesema Serikali imekuwa ikikosa mapato kutokana na kuibuka kwa wimbi la matapeli ambao wamekuwa wakiuza bima feki kwa wananchi .

Kauli hiyo imetolewa Jijini Mbeya na Meneja wa Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) kanda ya nyanda za juu kusini Bi,Consolata Gabone wakati wakifanya zoezi la ukaguzi wa bima kwa vyombo ya moto Jijini Mbeya.

Amesema watu hao ambao wengi wao hawana leseni za kufanya biashara ya bima wamekuwa wakifanya udanganyifu huo kwa wateja kwa kugushi bima na kuwazuia wateja wao jambo ambalo limekuwa likiikosesha serikali mapato.

“Makampuni yote ya bima yanawekeza kwenye tozo hivyo kuwepo kwa bima feki kunasababisha hasara kwa makampuni hayo ambayo yanashindwa kulipa tozo (VAT) za serikali kwa mujibu wa sheria.”Amesema Gabone 

Aidha amewataka watu wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha mara moja wizi huo kwani mkono wa sheria unawasaka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

“Mamlaka ya bima ipo kwa ajili ya kumlinda mwananchi na mkata bima kwani hasara za kutumia vyombo bila kuwa na bima vinampotezea haki muhanga wa ajali hasa katika suala la kufidiwa”Amesema Gabone

Meneja huyo wa kanda ya Nyanda za juu kusini ametoa wito kwa wafanyabiashara wa bima kufuata sheria na miongozo ya ufanyaji biashara hiyo kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya bima namba 10 ya mwaka 2009 na hivyo kuepusha usumbufu kwa wananchi wakati wanapotakiwa kupata fidia ya bima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...