Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 
 MTANGAZAJI wa Clouds na mmiliki wa mtandao wa Shafii Dauda, Shafii Dauda Kajuna,  na Benedict Kadege Jumatatu Septemba 24, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali. 
 Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka akisaidiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamewasomea washtakiwa shtaka lao mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina 
 Akiwasomea hati ya mashtaka Wakili Kombakono amedai kuwa kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda,  kinyume cha sheria walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 
Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hao wamekana huku upande wa mashtaka ukidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 
 Hata hivyo Wakili Jebra Kambole anayewatetea washtakiwa hao aliomba Wateja wake hao wapewe dhamana kwa sababu shtaka wanaloshtakiwa nalo linadhaminika. 
Wakili Kweka amedai kuwa hawapingi kutoa dhamana bali kama mahakama itaridhia kutoa dhamana izingatie kifungu cha 148 (6)(7) cha sheria ya makosa ya jinai. 
 Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mhina alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kwenye kitambulisho vya kuwatambulisha na barua ambazo zinatambulika. 
Pia kila mdhamini alitakiwa kusaini bondi ya Sh .milioni 15 na hawaruhusiwi kusafirisha nje ya Tanzania bila kupata kibali cha mahakama. 
 Pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafirisha mahakamani Oktoba 8 mwaka huu. Washtakiwa wamefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 8 mwaka huu.


 Baadhi ya watuhumiwa wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakiwa wameficha sura zao wamefika mahakamani hapo kwaajili ya kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.
 Gari la Jeshi la Polisi likiwafikisha watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwemo ya watumiaji wa maudhui ya matandao bila kibali. 
 Baadhi ya watuhumiwa wakiwa wameficha nyuso zao baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kwa  kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...