Mimi ni Abbu Omar, mwanamuziki mkongwe aliyewaji kupiga Bendi za Simba Wanyika / Les Wanyika kutoka 1981 – 1992. Pia nilishiriki katika recordings za Album nyingi maarufu kama “Mwana sikia”,  “Sikujua kama utabadilika”, “Haleluya”, “Shilingi yaua”, “Baba Asia”, “Mapenzi ni Damu”, “Mapenzi ya Weekend” na kadhalika.
Hivi sasa  Abbu Omar ameandika kitabu cha historia ya bendi za Wanyika kinachoitwa “ Maisha yangu na Bendi za Wanyika” Kuanzia bendi ya Young Nyamwezi Jazz 1958 (Tanga), Jamhuri Jazz 1964, Arusha jazz 1972, Simba Wanyika 1973, Les Wanyika 1978, Super Wanyika By Issa Juma 1981, Hadi mwisho wa Les Wanyika wakati wa kifo cha John Ngereza  mwaka 2002.
Kitabu hiki chenye kurasa 248 na picha za matukio mbalimbali, Kinapatikana:
Zanzibar Bookshop – Kariakoo jijini Dar es salaam – Shule ya Uhuru, Karibu na Ghorofa Kubwa la China Plaza
Simu: 0713 3523248
Mtaa wa Samora Opposite J-Mall njia panda ya Samora na Morogoro Road jijini Dar es salaam.
Simu: 0715520701
Mtoni Kwa Azizi Ally: Round About, Yerusalem Stationary, jijini Dar es salaam.
Simu: 0782387838 George
Mtoni Kwa Azizi Ally- Internet, Katika Fremu iliyopo kwenye Nyumba ya Mzee King Kikii.
Sheikh Hando - Simu 0719 529292
Mwananyamala – Komakoma karibu na Biashara Complex / Kambi ya Akudo Impact band
Simu 0715681838 - Timothy
Kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” cha Abbu Omar
Kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” cha Abbu Omar
Ankal akiwa na mtunzi wa kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” mkongwe Abbu Omar alipokuwa likizo jijini Dar es salaam mwaka 2010 akitokea nchini Japan alikokuwa akiishi na kufanya kazi
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na mumewe Bw. Khamsin (kushoto) na Keppy Kiyombile wa The Kilimanjaro Band Wana Njenje wakiwa na mtunzi wa kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” mkongwe Abbu Omar alipokuwa likizo jijini Dar es salaam mwaka 2010 akitokea nchini Japan alikokuwa akiishi na kufanya kazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...