Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii Mbeya
Mkurugenzi
wa Shule za Patrick Mission na mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela ametoa msaada
kwa wajane wawili katika kanisa la KKKT Forest Mkoani Mbeya .
Mwaselela
ambaye alipata nafasi ya kuzungumza na wanakwaya wa kwaya ya Safina ya kanisa
hilo, ambapo aliomba apewe wajane wawili Ili aweze kuwapa mitaji ya kujikwamua kimaisha.
“Mimi ni
Mtoto wa Mama ntilie ambaye nimefanikiwa leo hivyo niwaambie wazi, Mama yangu
alikuwa anauza Supu ili mimi nisome, hivyo nina kila sababu ya kuwasaidia watu mbalimbali wasiojiweza wakiwemp wajane,binafsi naona fahari kila ninapofika
mahali angalau niweze kuwagusa wanawake wawili” alisema Mwaselela.
Mwaselela
amesema kuwa mbali ya kuwa mtoto wa Mama Ntilie, walitokea watu wakainuka
wakanisomesha na wengine sasa ni wabunge na wamepata kushika nafasi za juu
serikalini.
Amesema kuwa
ni vyema watu wakajifunza kutoa na kusaidia wengine, kwani kwa kufanya hivyo
Mungu hugusa pale walipotoa na kuwabariki kwa kila hatua wanayopita.
Mwaselela
alimaliza kwa kusema ni vyema jamii ya Watanzania ijifunze namna ya
kusaidia wengine kwa kile kidogo wanachokipata katika shughuli zao za kila
siku.
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela akizungumza wakati wa Ibada katika kanisa la KKKT Forest Mbeya juu ya umuhimu wa utoaji kwa jamii.
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela, akikabidhi fedha kwa wajane ambao aliomba wasaidie katikati ya ibada
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela akiombewa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa KKKT Forest Mbeya.
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela akiagana na Mchungaji wa Usharika
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...