Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amepokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo 

Nditiye amewaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeona ni vema iwasilishe rasimu ya kanuni hizo ili ziweze kupata maoni ya wajumbe hao kwa kuwa mawasiliano ni suala la muungano. 

Aidha, amefafanua kuwa wajumbe walishiriki na kutoa maoni yao wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walishirikiana kutunga Sheria iliyoanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania na kufuta Kampuni ya Simu Tanzani ili kuiwezesha Serikali kumiliki Shirika hilo kwa asilimia 100 na liweze kujiendesha kwa faida kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa letu na ulinzi na usalama ambapo Shirika limeweza kutoa gawio kwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa Serikali.

Mhandisi Nditiye amewashukuru wajumbe wa Baraza hilo kwa ushirikiano wao wakati wa utungaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo Serikali imezingatia na kutekeleza maoni waliyoyatoa wakati wa utungaji wa sheria hiyo ikiwemo suala la uwakilishi wa Zanzibar kwenye Bodi ya Shirika na Ofisi Zanzibar

Amefafanua kuwa katika kifungu cha 7 (2) (b) cha sheria ya Shirika hilo, sheria imeelekeza wazi kuwa lazima wajumbe wawili wa Bodi ya Shirika watoke Zanzibar na muundo wa Shirika umezingatia uwepo wa Ofisi ya Shirika Zanzibar badala ya kuwa na tawi tu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Ahmed Salum wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (wa kwanza kushoto) akitoa maoni yake wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe. Mgeni Hassan Juma. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza kwa makini wasilisho na maoni ya wajumbe wa Baraza hilo wakati wa kikao cha kupokea maoni yao ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakisikiliza kwa makini maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar ya rasimu ya Kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...