Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji 
 Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni ameamuru Mkuu wa soko kuu la Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. John Ruzga kuwekwa chini ya ulinzi baada ya kutuhumiwa  kupokea fedha za wafanyabiashara kwa kigezo cha kwenda kuwalipia ushuru na kutozifikisha Halmashauri kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa Serikali kwa mtumishi wa umma. 

 Naye Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Baltazar Ngowi amwataka wafanyabiashara katika soko hilo kudai risiti pindi wanapolipa ushuru wa vibanda. 

 “Kutoa pesa bila kudai risiti pia ni kosa kisheria hivyo nichukue fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara mdai risiti pindi mnapolipa ushuru wa vibanda vyenu na mnapaswa kupeleka fedha zenu wenyewe badala ya kutuma mtu ili kuepuka kadhia ya kutapeliwa ” alisema Bw. Ngowi.

 Dkt. Madeni yupo katika wa muendelezo wa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ikiwa na lengo la kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, pia kuhakikisha wafanyabiashara wote na wamiliki wa vibanda wana leseni za muda husika, risiti halali za kodi na mikataba halali ya Halmashauri.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni (wa kwanza kushoto) akishuhudia ukaguzi wa daftari analotumia Mkuu wa soko kurekodi taarifa za wafanyabiashara jiji la Arusha, wakati wa muendelezo wa operesheni ya ukusanyaji wa mapato. 
Mfanyabiashara wa Soko Kuu Bw. Daniel Mushi (kushoto) na Mkuu wa Soko kuu la Jiji la Arusha Bw. John Ruzga wakati walipowekwa chini ya ulinzi katika operesheni hiyo ya ukusanyaji wa mapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...