Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuimarisha ulinzi uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga na Kata ya Vingunguti unaotarajia kufanyika Septemba 16 mwaka huu.

Limesema halitamvumilia mtu yoyote  atakayebainika kufanya kuvuruga katika mchakato huo na kwamba atakeyakamatwa matokeo ya uchaguzi atayasikia akiwa mikononi mwa Polisi.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza namna walivyoimarisha ulinzi katika maeneo ambayo uchaguzi mdogo.

Amesisitiza jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kabla, baada ya uchaguzi hadi matokeo yanapotangaza na mshindi kutangazwa.
“Napenda kuwatoa hofu wananchi jeshi la Polisi limejiandaa kwa kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo.

“Tunawaonya waliopanga kufanya vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Rai ya jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa siku ya hiyo na wahusika wa uchaguzi bila kuleta vurugu au wao kuwa chanzo cha vurugu,”amesema.

 Mambosasa ameongeza kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali kwa ajili ya kufanya doria kila sehemu wakiongozwa na askari maalumu wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Amewahakikisha jeshi hilo kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi chchote chenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akionesha bastola zilizokamatwa na jeshi la polisi katika msako wa wa kutafuta waharifu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Bastola na Magazini na Risasi zilizokamatwa katika msako wa waharifu Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na msako wa waharifu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...