Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya saratani nchini Dk.Dominista Kombe amesema saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza kwa kuua na kwamba kwa siku wagonjwa 80 wa aina mbalimbali  za  saratani hufariki dunia.

Ameishauri jamii na hasa  wanawake kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua iwapo wana tatizo la saratani au la huku akifafanua changamoto kubwa wagonjwa wengi wanafika hospitali wakiwa wamefikia hatua ya tatu au ya nne.

Dk.Kombe ambaye kwa sasa ni mstaafu na ameamua kuanzisha Dar es Salaam Oncological Care Clinic amesema hayo leo wakati anazungumza na wafanyakazi wa Benki ya Barclays kabla ya kuanza kuwapima saratani ya matiti.

Amefafanua ugonjwa wa saratani nchini umeshika kasi na saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoshika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili ni saratani ya matiti.

Amesema kibaya zaidi idadi kubwa ya wanaosumbuliwa na saratani hizo ni watu wenye umri chini ya miaka 60 na ipo haja ya kuchukua hatua mbalimbali ili kuepuka ugonjwa huo.

Amefafanua ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa  kupima afya mara kwa mara ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa elimu ya namna ambavyo mwanamke anaweza kupima saratani ya matiti.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (kulia), akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF).  
 Mshauri na mtaalamu wa masuala ya afya magonjwa ya saratani, Dk. Dominista Kombe (kulia) akionyesha jinsi ya kuangalia viashiria vya ungonjwa wa saratani ya matiti kwa baadhi ya wafayakazi wa Benki ya Barclays katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), jijini Dar es Salaam leo.
 Mratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Kisa Mwakatobe (kulia), akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki ya Barclays kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na taasisi hiyo.
 Mmoja wa waratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Gloria Kida (kulia), akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyougua ugonjwa huo pamoja na matibabu aliyoyapata wakati wa semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...