SERIKALI inatambua na kuthamini juhudi za wadau mbali mbali zinazofanywa zenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya Watanzania yanawezeshwa kikamilifu, hasa zinazochochewa na asasi za kiraia. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Watoto wa wizara hiyo, Margaret Mussai alipokuwa akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii ulioandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation.

Akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha asasi mbalimbali za kiraia, alisema Serikali inafarijika kuona wadau wakiungana na kupanga mikakati ya kufikia malengo ya mafanikio ya utendaji kwa pamoja kuihudumia jamii.

“...Asasi za kiraia mmekuwa muhimili muhimu kwenye kuhimiza maendeleo ya jamii, mmekuwa mnabuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi na kutoa huduma za maendeleo ya Jamii kwa kutumia gharama nafuu na hata muda mwingine kwa kutumia rasilimali za wanaojitolea,”

“...Tunatambua mchango wa asasi nyingi za kiraia zinazotoa elimu juu ya mapambano ya magonjwa yanayoambukizwa, mila na desturi zenye madhara kwa vijana wakiwemo watoto wa kike na wanawake. Lakini pia kuna asasi zinazowezesha vijana kuwekeza kiuchumi katika miradi midogomidogo ya uzalishaji mali,” alisema Ummy katika hotuba hiyo.

Aidha alisema licha ya Serikali kutambua mchango mkubwa wa asasi za kijamii, alizitaka kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na ushirikishwaji wa rika zote, huku zikizingatia sheria na katiba ya nchi ili kufikia malengo yao.
Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya An Nahl Trust.
Mwenyekiti wa Asasi ya An Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kilima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na asasi yake kwa kushirikiana na NAMA Foundation leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...