Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imeanza kutumia safari za anga kufanya doria katika kukabiliana na changamoto kubwa inayoikabili serikali katika uhifadhi wa Sekta ya misitu na maliasili kwa jumla.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo la doria hizo ni kuhakikisha ulizi unaimarishwa katika maeneo yote ya misitu ambayo TFS imepewa dhamana ya kuilinda.

“Nimeelekeza watendaji wangu kufanya doria ya anga kuanzia leo na tutaanza na Kanda ya Mashariki na nizitake kanda nyingine zijipange, maeneo/misitu korofi myabaini na kutafuta ramani zake. Nitawatumia ndege kwa ajili ya doria kutambua uharibifu.

“Tumekuwa tukifanya doria za misitu lakini tumekuwa tukiwiwa vigumu kuyafikia maeneo yote, lakini kupitia doria za anga sasa tutajua kila kinachoendelea kwenye eneo la misitu na kwa kutumia vikosi kazi vyetu tutafanya ulinzi kwa uhakika zaidi,” amesema Profesa Silayo.

Professa Silayo aliongoza kuwa ili kuongeza tija TFS itashirikiana na Wakuu wa wilaya pamoja wa wataalamu wa ardhi wa maeneo husika.

Akizungumzia mara baada ya kufanya doria ya anga, Meneja Msaidizi wa TFS, Kanda ya Mashariki, Bernadetha Kadala alisema doria hio imewawezesha kuona kwa karibu zaidi hali halisi ya misitu iliyopo kwenye Kanda za Mashariki na kufahamu kuna nini kinachotokea kwa wakati huo na hivyo itawawezesha kufanya ulinzi kwa weledi.
 TFS ikifanya doria ya anga ikionyesha baadhi ya wananchi wakiwa wanatengeneza jahazi kwa kutumia miti waliyovuna kinyume na taratibu kutoka msitu wa Mohoro River Wilayani Rufiji mapema jana. 
TFS ikifanya doria ya anga ikionyesha mistu wa Hifadhi wa Rufiji Delta ukiwa katika hali nzuri baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kuhifadhi mikoko kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. Picha na TFS.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...