Serikali imekubali kuongeza muda wa siku 43 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya daraja la nyerere kiunganishi cha barabara ya Kivukoni Kibada wenye urefu wa kilomta mbili ikiwemo kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF kumkata asilimia 0.01 mkandarasi wa kampuni ya China Railway construction engeneer Group katika malipo ya makubaliano ya ujenzi huo kutokana na uzembe wa kuchelewesha kukamilika kwa kazi ya ujenzi.

Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Ajira,vijana,sera bunge na wenye ulemavu) Mh Jenister Mhagama ameridhia wakandarasi hao kuongeza muda huo wa ujenzi kutokana na changamoto za kifusi ambacho awali kilishindikana kupatikana kutokana masuala kadhaa ikiwemo uharibifu wa mazingira katika eneo la Mbutu lilipo Kigamboni .

“Nimekubali ombi hilo kutokana na changamoto ya kifusi ambapo sasa kimepatiwa ufumbuzi na uongozi wa wilaya ya Kigamboni hivyo nataka katika muda huu niliuongeza barabara hii ikamilike haraka na wakazi wa kigamboni waweze kuondokana na changamoto hii ya barabara”alisema Mh Mhagama.

Mh Mhagama amesema kuwa barabara hiyo itakapokamilika itaweza kuongeza mapato zaidi kwa daraja na hivyo kukuza uchumi wa nchi kutokana na uwekezaji wa viwanda vingi katika eneo la kigamboni uliopo na unaoendelea kwa hivi sasa.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ndugu William Erio alimtaka mkandarasi kufanya kazi kulingana na mkataba na kwamba wataendelea kukata tozo ya adhabu ya kutokamilisha mradi kwa wakati na kwamba gharama zote zilizo nje ya mkataba hazitalipwa.

“Kama shirika tumeamua kumkata mkandarasi huyu kutokana na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati kama ilivypangwa awali na kuwa nitahakikisha nafuatilia hatua kwa hatua hadi ujenzi huu ukamilike ndani ya muda uliongezwa”alisema Erio.

Pia Mkurugenzi huyo wa NSSF alisema kwa sasa shirika hilo litaweka mfumo wa utambuzi wa vyombo vya usafiri kutoka kwa wakala wa serikali ili kuhakikisha mapato ya daraja yanaongezeka kutokana na uhalisia wa tozo halisi ya magari na kuachana na mfumo wa utambuzi kwa kutumia na njia ya kuhisi kwa kutumia macho. Ambapo amesema kuwa mfumo huo utaunganishwa moja kwa moja na mamlaka ya mapato TRA ili kuhakikisha kila gari linatozwa tozo kulingana na thamani ya gari.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigamboni wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana. 
 MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana.


Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) Jamal Mruma akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana, kushoto ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (aliyevaa kitenge) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana .


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana , kulia ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

 Eneo la kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni likiendelea na ujenzi wakatio Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana .Picha na MAELEZO.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...