Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MTANGAZAJI wa Clouds, Soudy Peter Kadio 'Brown' amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali. 
 Akisomewa mashtaka na Wakili wa serikali Mkuu Faraja Nguka kwa kusaidiana na wakili Estazia Wilson amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kati ya June 11 na September, 2018 ndani ya Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la SHILAWADU TV, mshtakiwa alitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka (TCRA). 
Hata hivyo, mshtakiwa Soudy Brown baada ya kusomewa shtaka hilo amekana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Wakili Peter Kibatala anayemtetea mshtakiwa huyo aliomba mteja wake apewe dhamana kwa sababu shtaka linalomkabili linadhaminika. 
 Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Rwizile amemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh.Milioni 2, pia mshtakiwa mwenyewe naye asaini bondi ya Sh.Milioni 2. Mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa. 
Kwa mujibu wa upande wa mashtka, wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi October 18, 2018.
Mtangazaji Soudy Brown

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanini mnaonyesha sura ya Soudy Brown wakati mwenyewe huificha? Acheni sifa za kijinga, Michuzi wewe ni mtu mkubwa kwenye tasnia hii. Vyombo vingine vyote vimeficha sura yake. Mmenifedhehesha sana kwa kiki hii ya kijinga. Ficheni sura yake tafadhali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...