Katika kutekeleza kwa vitendo jukumu la kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Tume ya Umwagiliaji ya Taifa (NIRC) ili kuchagiza kilimo cha umwagiliaji nchini.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema benki imejipanga kuchagiza tasnia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

“Ili kuninua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo nchini benki imejipanga kuwekeza mtaji wa kutosha katika kilimo cha umwagiliaji,” alisema.

Bw. Justine aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imeshatoa mkopo katika miradi 9 mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere alisema tasnia ya umwagiliaji ina mchango mkubwa katika kunyanyua uzalishaji nchini hatahivyo muitikio finyu wa wadau umekuwa ukirudisha nyuma tasnia hiyo.

Mhandisi Dkt. Matekere ameishukuru TADB kwa kuwa taasisi ya kwanza ya kifedha kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.

“uwekezaji huu wa pamoja utasaidia kuongeza uzalishaji hali itakayowaongezea kipato wakulima nchini na hivyo kusaidia kupunguza umaskini wa kipato kwa wakulima hasa wanaolima kwa kutegemea mvua,” alisema.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini. anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine.
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto) akiongea wakati wa kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Sheria ya TADB, Bibi Neema Christina John.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TADB wakifuatilia kwa makini utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini.  
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakitia saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakionesha makubaliano hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...