Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BARAZA la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Juu (THTU) limesema kuwa litaendelea kuwa na busara katika kufatilia madai yao kwa kufuata taratibu za Kiutumishi.

Baraza hilo lilikutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya stahiki zao katika vyuo vya umma nchini.

 Mwenyekiti wa  Taifa wa chama cha wafanyakazi Taasisi ya elimu ya juu (THTU) Dkt. Paul Loisulie akizungumza katika baraza hilo amesema kuwa serikali kuna vitu imefanya vizuri lakini vingine bado vinavyohusiana na madai hivyo busara lazima itumike.

Amesema kuwa kuna Mamlaka za serikali ambazo zipo kwa ajili yao ambazo zinatakiwa kuzifikia katika kupata ufumbuzi.

Dkt. Loisulie amesema kikao cha baraza ni cha dharula kwa wanachama kuwa na dukuduku kuhusiana  madai yao katika utumishi wa umma.
Aidha liosure ameeleza kwakina dhumuni la kikao hicho ni kutoa muelekeo juu ya maslahi ya wafanyakazi kwani wengi wao wamekua wakilalamikia masilahi ya malimbikizo ya mishahara ikiwa baadhi yao walishalipwa katika awamu zilizopita.

Dkt. Loisulie amesema madai hayo yalishapelekwa kwa sehemu husika na swala hilo litapelekwa pamoja na wataandaa walaka wa matatizo ya watumishi ili waweze kushughulikiwa. 

Mwenyekiti huyo amefafanua kuhusu sheria zilizojadiliwa ni pamoja na sheria ya bodi ya mikopo na wameona ipo haja ya  kupendekeza sheria na kanuni hizo kwa serikali ili kuboresha kanuni na sheria hizo kwa lengo la kuleta nafuu kwa watumishi.
 Mwenyekiti wa chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu (THTU) Dkt.John Loisulie  akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Chama hicho kuhusiana na madai mbalimbali ya masilahi ya Wafanyakazi wa taasisi ya Elimu ya Juu.

Viongozi wa THTU wakiwasikiliza wajumbe wa baraza hawapo pichani
Picha mbalimbali wajumbe wa baraza hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...