*Ni kwa ajili ya washindi wa Tulia Traditional Dances Festival 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust Dk.Tulia Akson ameushukuru Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kumkabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya washindi watakaopatikana kwenye tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018.

Dk.Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amekabidhiwa pikipiki hizo leo katika ubalozi huo na Mwakilishi wa Balozi wa China Tanzania nchini Xu Chen.Thamani ya pikipiki hizo ni Sh.milioni 21,600,000.

Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo Dk.Tulia amesema anaushukuru ubalozi huo kwa kutoa zawadi hizo kwa ajili ya washindi wa tamasha hilo litakalofanyika kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 22 mkoani Mbeya.

“Kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust tunatoa shukrani zetu kwa ubalozi wa China nchini Tanzania kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kwa kutoa zawadi kwa ajili ya washindi.

“Mwaka jana walitoa pikipiki 10 ambazo tulikabidhi kwa washindi.Lengo la tamasha hili ni kukuza utamaduni wetu na tumeanza na ngoma za asili.Pia  tunataka wanaoshiriki pia wajikwamue kiuchumi,”amesema Dk.Akson.

Akifafanua zaidi kuhusu zawadi kwa washindi Dk.Askon amesema mshindi wa kwanza kwa idadi iliyopo watapata zawadi na kwamba jumla ya vikundi 108 vitashiriki.

Pia amesema tamasha hilo ni endelevu na linafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na lengo kuu ni kukuza utamaduni wetu, pia iwe sehemu ya kuwawezesha wananchi kujenga uchumi,”amesema.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kutoka kwa Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akisainiana hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozini hapo jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jini Mbeya. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kwa ajili ya washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
(Picha na Muhidin Sufiani)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...