Na Khadija Khamis – Maelezo 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter amesema nchi yake itaendelea kuongeza ushirikiana wake na Tanzania katika masula ya Uchumi, Kijamii na Utamaduni. Balozi Frederic Clavieter alieleza hayo katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar Migombani alipofanya ziara ya kutembelea ofisi hiyo akiambatana na Maseneta watatu kutoka Ufaransa.

Maseneta waaliofutana na Balozi Clavieter ni Ronan Dantec kutoka Jimbo la Loire-Atlantique, Cyril Pellevat wa Jimbo la Haute-Savoie na Seneta Bernard kutoka Jimbo la Paris .Alisema katika kuimarisha ushirikiano huo, Ufaransa imeamua kuongeza msaada wake kwa Tanzania kutoka Euro milioni 50 kwa mwaka kufikia Euro milioni 100 ili kuharakisha maendeleo yake.

Alisema mahusiano kati ya Ufaransa na Tanzania ulianza muda mrefu uliopita na wananchi wa mataifa hayo mawili wamekuwa na ushirikiaano mkubwa katika masula ya Utamaduni kwa kushiriki katika Matamasha mbali mbali yanayoandaliwa na nchi hizo. Alisema ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo hivi sasa yameleta maafa makubwa katika baadhi ya nchi hasa nchi changa.

Balozi Frederec amefurahishwa na kuona vijana wa Zanzibar wanajifunza lugha ya Kifaransa na ameshauri vituo zaidi vya kufundishia lugha hiyo viongezwe ili kuimarisha zaidi Utamaduni wa nchi hizi mbili. Aidha alisema kujitokeza vijana wengi kujifunza Kifaransa kutawasaidia vijana hao kupata ajira kwani zaidi ya Watalii 20 elfu kutoka Ufaransa wamekuwa wakitembelea Zanzibar kutokana na vivutio vingi vya Utalii viliopo.


Rais wa Jumuiya ya Utamaduni ya Ufaransa na Zanzibar Khamis Abdalla Said akiwakaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter na maseneta watatu kutoka Ufaransa na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyofanywa na viongozi hao katika kituo cha Jumiya hiyo Migombani Mjini Zanzibar. 
Balozi wa Ufansa nchini Tanzania Frederic Clavieter akizungumza wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar iliopo Migombani Mjini Zanzibar 
Seneta Ronan Dantec kutoka jimbo la Loire-Atlantique akizungumza na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyoandaliwa na Jumuiya ya Ufarans na Zanzibar katia ofisi zao ziliopo Migombani Mjini Zanzibar 
wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar.

Wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar. 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...