Na Grace Semfuko- MAELEZO.
Ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini
Dar Es Salaam (Terminal 3) umekamilika kwa asilimia 81, na miezi minane ijayo kazi zote za ujenzi wa
majengo na mahitaji yote ya uwanja yatakuwa yamekamiliki na tayari usafiri wa anga wa Tanzania
kukidhi mahitaji yote ya kisasa kimataifa.
Ujenzi huo unaojengwa na kampuni ya Bam International ya Uholanzi ikisaidiwa na kampuni zingine 21
za kihandisi za ndani na nje ya nchi, ujenzi ulianza Juni mwaka 2013 na utakamilishwa Mei 31, 2019 kwa
gharama Yuro 254 milioni, sawa na shilingi Bilioni 560 za kitanzania.
Akizungumza uwanjani hapo Msimamizi wa Jengo hilo kwa upande wa Mradi huo kutoka Wakala wa
Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Burton Komba, amesema ujenzi huo unaendelea vizuri na
kwamba kukamilika kwake kutarahisisha kusafirisha Abiria wa Kimataifa ambao kwa sasa
wanahudumiwa na Uwanja huo jengo la pili (Terminal 2).
“Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jengo la tatu utakamilika mei 31 mwakani ambapo utahudumia Abiria
milioni 6 kwa mwaka,hii itasaidia kuhudumia abiria wengi zaidi ambao walikuwa wakihudumiwa na
Terminal 2, (jengo la pili)”.
Kukamilika kwa uwanja huu wa jengo la tatu ambapo huduma zote zimewekwa katika viwango vya juu
vya kimataifa na hivyo jengo hilo kutumika kutoa huduma za viwango vya kundi la watu muhimu (VIP) na
watu mashuhuri kibiashara (CIP).
Mhandisi amesema wakati jengo la pili linajengwa lengo lilikuwa ni kuweza kumudu abiria milioni moja
na nusu lakini akasewma kwa sasa jengo limekuwa likihudumia zaidi ya idadi hiyo, “tumekuwa tukifikia
abiria milioni mbili na nusu” alisema Mhandisi Komba.
Jengo hilo la tatu litakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege 17 hadi 19 zikiwemo ndege kubwa kwa
wakati mmoja na hivyo kumudu abiria hadi milioni 6 kwa mwaka, pia eneo la nje ya uwanja kuna nafasi
ya kuegesha magari 2,000 kwa dhamira ya kushusha na kupakia abiria wanaokuja na kuondoka nchini.
Kukamilika kwa ujenzi huo ni juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha miundombinu
inaboreshwa, lengo likiwa ni kufanikisha usafiri wa anga kasasa zaidi ili kuleta tija kwa uchumi wa
Tanzania toka abiria na mizigo ya ndani na mataifa mbalimbali duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...