Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza hali ya afya katika jimbo la Manonga na hii ni baada ya mikakati ya kuboresha huduma za afya katika vijiji vyote  Jimboni  humo.

Akifanya mahojiano na blogu ya jamii Gulamali amesema kuwa: "Ni furaha yetu kuona Upasuaji unafanyika katika vijiji vyetu na tuna washukuru Afrikan Dev Bank kwa kufanikisha hili. Kituo cha afya cha Choma  Chankola tayari kimeshafanya  upasuaji 69 na kati ya 69 ni 1 tu ndio iliyofeli na  hiyo ni kutokana na  mzazi kuchelewa kufika Kituoni hali iliyopelekea Upasuaji wake kufanikisha mtoto mmoja na mama kuwa hai na mtoto mwingine kupoteza maisha, lakini zilizobaki zote 68 zilienda Vizuri" ameeleza Gulamali.

Kuhusiana na huduma za upasuaji zinazopatikana katika Kituo hicho cha Afya Gulamali amesema ; "Upasuaji wa kutoa mawe tumboni, kujifungua, na upasuaji kwa  watoto na huduma zote hizo zinafanyika katika kituo chetu cha afya Choma" ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa hayo ni maendeleo makubwa sana, kilichobaki ni kuongeza majengo hasa ya mama na mtoto, jengo la kuhifadhia  maiti, maabara, jengo la Ufuaji na Nyumba za Watumishi na hiyo ni  Sambamba na kuongeza madaktari na wauguzi.Hata hivyo anamshukuru Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake kwa kutoa Fedha za Kuboresha Kituo hicho cha Afya cha Choma Chankola.

 Pia amesema kuwa; "Ni matumaini yetu Tutaweza pata hela kwa ajili ya hayo majengo, na  nitumie nafasi hii kumpongeza Daktari Frank na wauguzi wote kituoni hapa kwa huduma zao wanazotoa" ameeleza.

Baadhi ya wananchi wamempongeza Mbunge huyo na kueleza kuwa amekuwa lulu kwa wana Manonga hasa kwa kutoa vipaumbele muhimu kwa Wananchi bila kujali itikadi zao na wamemtaka kuendelea na moyo na imani hiyo ya kuipeleka Manonga mbele zaidi.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya majengo katika hospitali ya Choma Chonkola katika jimbo la Manonga.
Muonekano wa chumba cha upasuaji katika hospitali iliyopo katika kijiji cha Choma Chonkola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...