Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya sh.milioni 41 katika Chuo cha Ufundi Maalumu Yombo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga amesema kuwa vifaa hivyo vimekwenda kwa watu muhimu katika kuwaandalia maisha ya baadaye kwa vijana wenye ulemavy mbalimbali.

Amesema kuwa msaada huo sio mwisho kutokana na mahitaji ya Chuo hicho kutoa elimu kwa vijana wenye mahitaji maalum kwani serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda ambapo vijana wanaweza kuunda vikundi na kuanzisha viwanda na kuweza kujipatia kipato na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Dkt Mwesiga amesema vifaa hivyo lazima vitumike kwa malengo ualiyokusudia ikiwa ni kujifunzia wanafunzi hao na kupata ujuzi wanaohitaji pamoja na kanda ya VETA kufatilia vifaa hivyo na maendeleo ya wanafunzi katika Chuo cha Yombo.

“Nia ya serikali ni kuona watu wenye mahitaji maalumu wanapata ujuzi kutokana na ulemavu wao na hakuna kuachwa nyuma jamii hiyo na wala kubaguliwa kwa kuwakosesha elimu”amesema Dkt. Mwesiga.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga amesema kuwa maombi ya Chuo cha Yombo yalikuwa yanamkosesha usingizi kwa kutambua vijana waliopo wana mahitaji maalum ikilinganishwa na maombi mengine.

Picha ya Pamoja Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga pamoja Kanda ya VETA Dar es Salaam,Watumishi wa Chuo pamoja na wanfaunzi.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akizungumza wakati hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Maalum Yombo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa akitoa historia fupi ya chuo hicho katika hafla iliyofanyika Chuoni hapo o jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akikabidhi moja kifaa cha msaada kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufiundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa katika hafla iliyofanyika Chuo hapo , jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...