Pichani ni baadhi ya vijana wa zamani waliopitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria kambi ya Ruvu JKT (832KJ) Oparesheni Kambarage 1990/91 wakiwa pamoja baada ya kuhudhuria sherehe za kumaliza jeshi vijana kwa mujibu wa Sheria Oparesheni Mererani Ijumaa Septemba 14 kambini Ruvu.

Hii ni miaka 27 tangu vijana hao wa zamani kupitia mafunzo kambini hapo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa wa zamani aka makuruta wa zamani  Be Ameir Juma Nondo, umoja huo una mpango wa kurudisha fadhila kambini hapo kwa kutoa mchango katika kambi na kijiji Jirani na kamba hiyo kwa kuwa eneo hilo lina kumbu kumbu kubwa katika ujenzi wa maisha ya vijana hao waliopita hapo . 
 Be. Nondo ametaja miongoni mwa mambo waliyojifunza kambini hapo ni pamoja na uzalendo kwa nchi yao, ujasiri katika maisha, upendo na mshikamano katika jamii pamoja na kujituma, kuchapa kazi kwa bidii, utiifu na umakini katika kazi na maisha kwa ujumla. 
 Mgeni rasmi katika sherehe za ufungaji mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Joketi Mwegelo amewataka vijana hao kuepuka kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwani kuna Sheria ya Makosa ya mtandao inaweza kuchukuliwa dhidi yao. 
 Aidha, mgeni rasmi hiyo amewataka vijana waliomaliza mafunzo hayo kuwa wazalendo , watiifu, wachapakazi, waadilifu na mabalozi wazuri popote watakapokwenda kuitumikia nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...