VYAMA vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha
demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi
imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha
kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.
Hayo yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji
Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa
vyama vya siasa kinachoendelea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea
vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze
kujiendesha kama taasisi.
Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga
vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika
vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu
kutoka Ofisi yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali.
‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile
mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni
vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji
wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji
Mtungi.
Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa
kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili
linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.
Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Francis Mutungi akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Msajili msaidizi Sisty Nyahoza akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa katika semina ya siku mbili leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam
Profesa Rwekaza Mkandala akizungumza na viongizi wa vyama vya siasa kuhusu jinsi ya kujiendesha chama kama taasisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...