Na Tiganya Vicent
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Tabora kufanyakazi kwa ushirikiano na uzalendo ili kuimarisha ulinzi wa eneo lao na nchi kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Sharif Othman wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Tabora na zile za Wilaya zake wakati ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Alisema ushirikiano utawasaidia kuwafanya kuwa kitu kimoja na kuwa nguvu ya pamoja katika kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi na nchi kwa ujumla.

Meja Jenerali Othman alisema viongozi wa vyombo hivyo wanapaswa kujenga tabia ya kutembelea na kushirikiana katika shughuli mbalimbali kama vile michezo na sherehe kama sehemu ya kujenga mshikamano ambao ndio utawasaidia kuwa kitu kimoja katika ulinzi wa nchi.

Alisema hali hiyo itawasaidia kupeana taarifa kama kutakuwepo na jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi na hivyo kuchukua hatua za pamoja na haraka katika kulikabili.

“Sisi tuwe mashine ya kuwezesha usalama wa raia nan chi kwa kupeana taarifa na kushirikiana” alisema.

Mkuu huyo wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi aliongeza kuwa sio vema kugonja tatizo litolekee ndio taarifa itolewe bali taarifa inapaswa kutolewa mapema ili kuzuia tatizo.

Aidha Meja Jenerali huyo alitoa wito kwa wananchi kuwa karibu na majeshi yao kwa kutoa taarifa zote ambazo zinahatarisha usalama wa nchi ili kama kuna wahusika waweze kuchukuliwa hatua mapema kwa usalama wao na nchi kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...