Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WANANCHI wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini katika hifadhi za misitu nchini wametakiwa kutii sheria za uhifadhi na kujiepusha na vitendo viovu vya uharibifu wa mazingira vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili na kutishia nchi kuwa jangwa.

Hayo yamesemwa Septemba 23, 2016, Mkoani Geita na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Professa Dos Santos Silayo wakati akizungumza na viongozi wa migodi ya dhahabu iliyopo katika Shamba la miti Biharamulo mkoani humo.

Alieleza kuwa vitendo hivyo vya uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukataji wa miti hovyo, kilimo, uchungaji holela wa mifugo, uanzishaji makazi na shughuli zingine za kibinadamu katika shamba hilo linalotarajiwa kuwa shamba la pili kwa ukubwa nchini likifuatia kwa shamba la miti la Sao Hill lililopo Mafinga mkoani Iringa.
"Uharibifu wa misitu mnaofanya mgodini hapa unatisha! Uchimbaji wenu unateketeza miti lakini mbaya zaidi mnatumia tekinolojia duni inayowalazimu kutumia miti mingi mnayovuna kinyume na taratibu kuzuia mmomonyoko wa udongo katika mashimo mnayochimba madini.
“Endapo mkiendelea na kasi hii mtaigeuza nchi kuwa jangwa, na hili hatuwezi kulifumbia macho! Tekelezeni mpango wa usimamizi wa mazingira, na hili linawezekana, jana nilipita katika msitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ‘Council’ ambapo uchimbaji madini unafanyika na wachimbaji wadogo. Kazi nzuri wanaifanya na mwekezaji anatekeleza vizuri mpango wa usimamizi wa mazingira. Miti bado imesimama na mashimo hufukiwa baada ya utafutaji kukamilika,” anasema Professa Silayo.

Katika utekelezaji na usimamizi wa sheria hizo za uhifadhi, aliwataka watumishi wa TFS kusimamia sheria hizo kila siku na kuendesha utekelezaji wake kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya na Mikoa ili kuimarisha utekelezaji wa sheria hizo na kuweka uwazi katika utendaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Injinia Mtemi Msafiri Simion
 alisema wilaya yake inakabiliwa na uhaba wa ardhi uliosababishwa na ongezeko kubwa la watu waliovutiwa na shughuli za kiuchumi hasa uchimbaji wa madini ambapo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ni changamoto kubwa katika uhifadhi wilayani humo.

“Wachimbaji wadogo wa madini wanakata miti, wanakatwa hasa lazima sasa tuweke sheria kali kuhakikisha wamiliki wa migodi hawaruhusiwi kufanya shughuli zao pasipo kuwa na shamba ya miti na wakati wakingoja miti yao kufikia umri wa kuvunwa lazima waeleze walikovuna miti wanayotumia kufanikisha uchimbaji wao kuthibiti uharibifu wa misitu,” alisema

Shamba la miti Biharamulo ni miongoni mwa mashamba manne ya Serikali yaliyoanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika mwaka wa fedha 2017/18 likiwa na ukuwa wa hekta 69,758 ambapo jumla ya miche 495,506 ilipandwa kwenye hekta 446 mwaka 2017, ikiwa ni mwaka wa kwanza wa upandaji katika Shamba hilo.
Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Professa Dos Santos Silayo akitazama moja kati ya mashimo yanayochimbwa madini ya dhahabu katika Shamba la Miti Biharamulo jana. Mashimo hayo yanatumia magogo mengi ya miti yanayovunwa kinyume na taratibu kuzuia udongo kumong’onyoka hali inayohatarisha uhifadhi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...